Posts

Showing posts from May, 2020

Shule ya sekondari yapewa jina la Jokate Mwegelo

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ambayo inajengwa na kampeni ya Tokomeza Zero kupitia Harambee ambayo iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam na DC Jokate baada Jumamosi hii kutembelea na kujionea kazi kubwa iliyofanyika katika shule hiyo aliyoipa jina la Jokate Girls High School iliyopo Mhaga wilayani Kisarawe. . Waziri baada ya kuona ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia 70, alimpongeza DC Jokate huku akidai ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kubwa nchini Tanzania. Pia alimtaka Mkurugenzi wa Kisarawe, shule hiyo ambayo mpaka sasa ina madarasa nane ya kisasa, maabara moja, bweni moja la wanafunzi 100 pamoja na nyumba moja ya mwalimu kuipa jina la Jokate Girl Secondary kutokana kazi kubwa iliyofanya na mkuu huyo wa wilaya.

Kifo cha George Floyd: Maandamano yatanda kote Marekani kudai haki

Image
Waandamanaji wakusanyika nje ya Ikulu pamoja na maeneo mengine juu ya kifo cha raia mweusi George Floyd. Waandamanaji wanakabiliana na polisi katika miji mbalimbali nchini Marekani juu ya mauaji ya raia mweusi wa Marekani ambaye hakuwa na silaha aliyekufa mikononi mwa polisi huko Minneapolis. Gavana wa Minnesota amesema kwamba kifo cha George Floyd aliyekuwa kizuizini kimeonesha mauaji ya kiholela. New York, Atlanta na maeneo mengine yamekuwa yakishuhudia ghasia huku Ikulu ya Marekani ikiwekewa katika hatua ya kusalia ndani kwa muda mfupi. Aliyekuwa afisa wa polisi katika eneo la Minneapolis ameshtakiwa kwa mauaji kutokana na kifo hicho.     Hali ilivyo hadi kufikia sasa? Katika mji wa New York, eneo la Brooklyn, waandamanaji walikabiliana na polisi kwa kuwarushia chochote walichoona, kuwasha moto na kuchoma moto magari ya polisi. Maafisa kadhaa wa polisi walijeruhiwa. Mayor Bill de Blasio aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter: "Hatutaki kushuhudia usiku mwengine kama huu.&qu

Hali mbaya ya hewa imeilazimu NASA kuahirisha safari

Image
Hali mbaya ya hewa imeilazimu kampuni ya wanasayansi wa anga ya SpaceX kusitisha uzinduzi wa chombo cha Nasa astronauts Doug Hurley na Bob Behnken katika kituo cha anga cha kimataifa (ISS). Wanaume hao wawili walikuwa wana nia ya kwenda kwenye kituo cha anga cha Kennedy ambapo inadaiwa kuwa jaribio la kwanza katika kituo cha anga ya juu kufanyika Marekani tangu miaka 9 iliyopita . Lakini hali mbaya ya hewa ilisababisha waongozaji wa mitambo kusitisha uzinduzi huo, dakika 16 kabla ya roketi hizo kuanza safari. Fursa nyingine ambayo SpaceX na Nasa wanayo ni kufanya jaribio jingine Jumamosi. Na kama haitawezekana, watapata fursa nyingine Jumapili. Changamoto ya hali ya hewa ilianza saa moja kabla ya muda wa uzinduzi kufika. Lakini maamuzi ya kubadili uzinduzi yalikuwa ya ghafla wakati ambao roketi ya SpaceX Falcon na kikosi chake cha Dragon walikuwa wanapaswa kuondoka katika muda uliopangwa la sivyo wangeshindwa kufika katika muda kukipata kituo cha anga cha kisayansi. Hii inamaanisha kuw

Ajuza wa miaka 103 apona Virusi vya Corona, ajipongeza kwa bia baridi

Image
Ajuza mweye umri wa miaka 103, Jennie Stejna amejipongeza kwa kunywa bia ya baridi aina ya Bud Light, baada ya kupona ugonjwa wa Virusi vya Corona. Bibi huyo anayepatikana Massachusetts Jijini Boston, alianza kuumwa ugonjwa huo mwanzoni mwa mwezi Mei, kwa dalili za kukosa ladha pia na kuumwa na homa kisha kupelekwa hospitali. Kwa mujibu wa TMZ, Daily Mail na vyombo vingine vya habari, Akitoa taarifa hiyo mkwe wa mjukuu wake Adam Gunn amesema, wote walikuwa wanajua tayari wanaelekea kumpoteza bibi yao, na kuna siku aliwahi kumuuliza kama yupo tayari kwenda mbinguni kisha bibi akamjibu ndiyo.Mzee huyo kwa sasa ni mjane na mumewe alifariki mwaka 1992 akiwa na miaka 82, amebahatika kupata watoto wawili, wajukuu watatu, vitukuu wanne na vilembwekezi wanne.

WHO “Dawa ya Corona anayopendekeza Trump Hydroxychloroquine ni hatari kiafya”

Image
Majaribio yanayofanyiwa dawa ya ugonjwa wa malaria Hydroxychloroquine ili kuona iwapo inaweza kutibu virusi vya corona yamesitishwa kutokana na hofu ya usalama wake, shirika la afya duniani WHO limesema. Vipimo vilivyokuwa vikifanywa katika mataifa kadhaa vimesitishwa kwa muda kama hatua ya kuchukua tahadhari, lilisema shirika hilo siku ya Jumatatu. Hatua hiyo inajiri baada ya utafiti wa tiba uliofanyika hivi karibuni kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuongeza hatari ya mgonjwa kufariki kutokana na virusi hivyo. Rais Donald Trump amesema kuwa anatumia dawa hiyo kuzuia virusi hivyo. Rais huyo wa Marekani ameikuza dawa hiyo ya malaria, kinyume na ushauri wa kimatibabu na onyo kutoka kwa maafisa wa Afya kwamba inaweza kusababisha tatizo la moyo. Rais Trump alizungumzia kabla kuhusu matumizi ya dawa hizi kwa ajili ya Covid-19 Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins vifo vilivyotokana na corona vimefikia 98,218. Wiki iliopita, utafiti uliofanywa na jarida la tiba duniani Lancet ulibaini kw

Yaelezwa huyu ndio mwanamke aliyepigwa busu mara nyingi zaidi duniani

Image
Wakati fulani katika karne ya 19, mwili wa msichana mdogo ambaye alikuwa amekufa maji uliokolewa katika mto Seine. Kama ulivyokuwa utamaduni wakati huo, mwili wake ulikuwa wazi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha mjini Paris, kukiwa na matumaini kwamba huenda mtu anaweza kuuona na kumtambua, lakini hakuna aliyemtambua. Katika picha hii ya maelezo iliopigwa mwaka 1816, watu wanaonekana wakitembelea chumba cha wafu wakitazama miili , kitu kilichopendelewa sana wakati huo. Daktari wa upasuaji aliyekuwa katika zamu alivutiwa na tabasamu ya uso wa msichana huyo hatua iliomfanya kumuomba mtengenezaji mask au barakoa kuunda uso kama wake. Ni kutokana na hatua hiyo ndiposa uso huo wa mwanamke aliyefariki ulihifadhiwa milele. Uso kuhifadhiwa. Wengi wao wanaelezea hadithi hiyo ya msichana asiye na hatia anayewasili mjini Paris kutoka mashambani , anatongozwa na mtu tajiri na kuwachwa anaposhika ujauzito wake . Baada ya kukosa mtu wa kumsaidia , anajirusha katika mto Seine. Lakini kuna hadithi

Virusi vya corona: Mashine ya kupima corona 'yakutwa na hitilafu Tanzania'

Image
Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza kwamba uchunguzi wa serikali uliokuwa ukifanywa katika maabara kuu ya nchi hiyo umebaini kuwa moja ya mashime ya kupima corona ilikuwa na hitilafu. Waziri Ummy Mwalimu hii leo ametangaza matokeo ya uchunguzi aliyoagiza kufanyika baada ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kutilia shaka ufanisi wa maabara hiyo. "Kamati imebaini kuwepo kwa mapungufu ya uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo na uhakiki wa ubora wa majibu'' amesema Waziri Mwalimu. Pia kumebainika kuwepo kwa udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya covid-19, aidha imebainika kuwepo kwa upungufu wa Wataalamu"- Waziri Afya Ummy mwalimu amesema. Wizara ya afya nchini humo imeweka wazi kwamba sasa vipimo vitakuwa vinafanyika katika maabara iliyopo mabibo. "Kuanzia sasa shughuli zote za upimaji wa maabara ya taifa zitafanyika katika maabara mpya ya mabibo yenye vifaa vya kisasa vyenye ubora na uwezo wa kupima sampuli 1,800 ndani ya saa 24"- amesema Um

Simba yafungua website yao rasmi, Manara na Senzo wafunguka wachezaji waliosajili pia mazoezi ya timu kuanza rasmi siku hii

Image
Akiongea C.E.O wa klabu hiyo @football_senzo pamoja na msemaji wa klabu hiyo @hajismanara wametolea ufafanuzi juu ya Website hiyo ya Simba ambayo utakuta historia ya klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na Matokeo I ya michezo yote ambayo Simba imewahi kucheza, kwa maana nyingine taarifa zote za klabu hiyo tena kwa lugha mbili KISWAHILI na KIINGEREZA. Mbali na hilo C.E.O bwana @football_senzo amesema kuwa kuna taarifa nyingi sana na amekuwa akipokea simu nyingi za mawakala kuhusu usajili mpya na kusema kuwa lengo lao kwa sasa ni kupeleka nguvu zao kwenye ligi wahakikishe wanashinda taji hilo kwani wapo kileleni mwa ligi lakini pia kupelekea macho na nguvu zao kwenye ligi ya AZAM FEDERATION na kuhakikisha wanafanya vizuri na baada ya hayo yote basi taarifa na wachezaji waliosajili watatangazwa rasmi.

Mfahamu Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Image
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye anatoka Chama cha Mapinduzi, kitaaluma ni mwalimu na mtalaamu wa kemia. Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania. Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi huko huko Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1975 na baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza mwaka 1977 hadi 1978. Kiongozi huyo alijiunga na chuo cha ualimu cha Mkwawa kilichoko Iringa, Kusini mashariki mwa Tanzania kati ya mwaka 1979 na 1982 ambapo alitunukiwa Stahahada ya Ualimu. Baada ya kufuzu, alifundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbalimbali za sekondari kuanzia mwaka 1983. Magufuli hakuishia hapo kielemu kwani aliamua kujiendeleza zaidi na kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 hadi 1988 ambapo alitunukiwa shahada ya ualimu katika masomo ya kemia na hisabati. Baadaye, aliamua kukolea katika kemia na akarejea chuoni na kusoma hadi ngazi ya udaktari. Siasa za Tanzania Katika s

”Vyuo, michezo ruksa 1/06/2020, watalii kuingia nchini mwezi huu,”- Rais Magufuli

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 mei 2020 amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni. Viongozi hao walioapishwa ni 1. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake Wazee na Watoto. 2. Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani. 3. Dkt. Jacob Gideon Kingu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria 4. Balozi Mteule Phaustine Martin Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji 5. Balozi mteule John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya 6. Brig. Gen. John Julius Mbungo kuwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU. Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. Katika ghafla hiyo rais Mugufuli amesema kuwa kuanzia tarehe 1/06/2020 Vyuo vyote vifunguliwe, vijana waliokuwa kidato cha sita ambao wanajiandaa kwenye mitihani yao, nao kurudi mashuleni huku michezo nayo ianze tena kwa ligi mbalimbali hapa nchini. Wakati nd

Rais Magufuli “Haiwezekani kila dereva anayeenda Kenya ana Corona, Mbona dereva wangu hana”

Image
“Haiwezekani kila Dereva ambaye anaenda Kenya awe na corona, mimi nina Dereva wangu hapa kwahiyo na yeye ana corona?, Dereva fungua dirisha la gari wakuone.. haya Watu wa Singida mnamuona huyu dereva  “Corona ipo lakini naamini itaisha tu, lakini kikubwa tusiogope na wala tusitishane, hapa Singida naona hamjawa na hofu ndio maana waliovaa barakoa wachache, hata mimi sijavaa, Mkuu wa mkoa pia hajavaa, tuombe Mungu, tuchukue tahadhari lakini tuchape kazi”

Corona: Hauwezi kukimbia kifo, baa, hotel na biashara zote zifunguliwe – RC Makonda

Image
RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida. Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo. “Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea, Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwaiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida” Alisema RC Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waende

Habari Njema: Chanjo mpya ya corona yaonyesha matokeo mazuri kwa muda mchache

Image
Kampuni ya Moderna katika taarifa yake imesema majaribio waliyafanya katika watu 8 waliojitolea wenye afya walipata chanjo yake ya majaribio ilikuwa salama na ilichochea majibu na kuimarisha kinga ya mwili. Imewekwa kwenye ratiba ya kasi ya kuanza majaribio makubwa ya wanadamu hivi karibuni. Chanjo ya kwanza ya coronavirus kupimwa kwa watu inaonekana kuwa salama na inayoweza kuchochea majibu ya kinga dhidi ya maambukizo, mtengenezaji, Moderna, alitangaza Jumatatu, akiwapa matumaini ulimwengu wa kutamani njia za kukomesha janga hili. Matokeo ya awali, katika watu wanane wa kwanza ambao kila mmoja alipokea dozi mbili za chanjo ya majaribio, lazima sasa irudishwe katika vipimo vikubwa zaidi katika mamia na halafu maelfu ya watu, ili kujua ikiwa chanjo hiyo inaweza kufanya kazi katika ulimwengu. Teknolojia ya Moderna, inayojumuisha nyenzo za maumbile kutoka kwa virusi inayoitwa mRNA, ni mpya na bado haijatoa chanjo yoyote iliyoidhinishwa. Habari za mapema za kuahidi zilituma hisa za Modern

Mchungaji Kyashama “Upinzani kazi yao kuiongelea vibaya Serikali wanatia aibu, Rais Magufuli anapewa maono na Mungu”

Image
Mwanasheria John Simon Kyashama ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la River of Healing Ministry lililoko kiluvya kwa komba ameta maoni yake kuhusu Hotuba ya Rais Magufuli na kumpongeza. Mchungaji Kyashama “Upinzani kazi yao kuiongelea vibaya Serikali wanatia aibu, Rais Magufuli anapewa maono na Mungu” –  Mwanasheria John Simon Kyashama ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la River of Healing Ministry lililoko kiluvya kwa komba ameta maoni yake kuhusu Hotuba ya Rais Magufuli na kumpongeza. mbali na kumpongeza rais Magufuli kyashama aetumia fursa hiyo kuwashauri viongozi wa Upinzania kuwa waache kupingana na Serikali na badala yake waungane ili kutokomeza Corona. Kyashama ameongeza kuwa Rais Magufuli ameuonyesha ulimwengu kuwa yeye ni Mwana Sayansi na ana uelewa wa kisanyansi, Mfano Rais Maguful;i akitoa hotuba hata WHO shirika la Afya duniani wanarudia yale yale.

Bundesliga kuanza kutimua vumbi kesho, Dortmund kuwavaa Shalke 04

Image
Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inarejea tena mwishoni mwa juma baada kusitishwa kwa karibu miezi miwili kutokana na janga la virusi vya corona. Kuanza tena kwa ligi hiyo kunaangaliwa kama jaribio juu ya iwapo kandanda na mashindano mengine ya michezo duniani yanaweza kuanza tena chini ya kiwingu cha janga la COVID-19. Miongoni mwa michezo ya kufungua dimba itayofanyika kesho ni pamoja na mpambano wa kukata na shoka kati ya mahasimu wa jadi Borussia Dortmund na Shalke 04 mjini Dortmund. Hata hivyo mechi tisa za duru ya 26 ya Bundesliga zitachezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani. Ligi nyingine barani Ulaya ikiwemo ile ya Uingereza, Italia na Uhispania zinatarajiwa kuanza tena baadae mwezi Juni.

Virusi vya corona: Mtaalamu wa chanjo 'aliyefutwa kazi' asema Marekani itakabiliwa na hali mbaya zaidi katika majira ya baridi

Image
Afisa wa zamani wa ngazi ya juu wa afya nchini Marekani ameliambia bunge la kongresi kuwa nchi inaweza kukabiliwa na "kipindi kibaya zaidi cha majira ya baridi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya hivi karibuni " kwa sababu ya virusi vya corona. Rick Bright aliongoza shirika la serikali kujaribu kutengeneza chanjo,lakini akaondolewa katika kazi hiyo mwezi uliopita. Awali alisema aliondolewa kazini kwa kuelezea hofu juu ya tiba zinazotangazwa na rais Donal Trump. Rais Trump alimfuta kazi kwa madai kuwa alikua mtumishi "asiyeridhika" Bwana Bright pia aliiambia kamati ya Bunge la wawakilishi ya masuala ya afya kuwa ''maisha yanapotea'' kwa sababu ya serikali "kutochukua hatua " katika hatua za mwanzo za mlipuko wa virusi vya corona. Alisema kuwa kwa mara ya kwanza alizungumzia juu ya ukosefu wa zana za matibabu mwezi Januari, na kufikisha suala hilo katika "ngazi za juu" za Wizara ya Afya na huduma za binadamu (HHS), lakini "ha

ZAWADI YA MAISHA

Image
Ni tarehe 16 Novemba tena! Mvua zinanyesha kama ilivyokuwa katika siku kama hii miaka 45 iliyopita. Natamani ungekuwepo ili ushuhudie kinachoendelea sasa hivi katika kusanyiko hili kuu, lakini haiwezekani…. Haiwezekani Aurelia..!!! Aureliaa….. mwanamke wa ndoto zangu, mwanamke uliyenitambulisha kwenye dunia ya mapenzi…nitawezaje kukusahau ewe muhebi wangu! Nakumbuka tarehe kama hii mwaka ya 1968, ndiyo ilikuwa tarehe ambayo mimi na wewe tuliangukia penzini. Naikumbuka sana siku hiyo, ni siku ambayo nilikuwa natoka kuuza maziwa kwenye Senta ya kijiji chetu, mara ghafla mvua ikanikutia njiani kabla sijafika  nyumbani kwetu, nikaja kujibanza upenuni mwa nyumba yenu ili kujikinga nisilowe. Hapo nikakutana na wewe ukiwa unakinga maji ya mvua ile, kutokana na kunyeshewa sana… gauni lako lililowa na kushikamana na mwili wako na kuyafanya maungo yako yajichore juu ya gauni lile. Chuchu zako za saa sita zilizochongoka mithili ya miba, zilikuwa kama vile zinang’ang’ana kutoboa gauni lako bila ma

Ni vita ya fedha Tottenham dhidi ya Arsenal kuwania saini ya Willian, wengine sokoni

Image
Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, raia wa Nigeria atarejea klabu hiyo baada ya kuchezea Manchester United kwa mkopo kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya China ambayo imepangiwa kuanza mwezi Julai. (Sky Sports) Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, atarejea klabu hiyo kutoka Manchester United Huku hayo yakijiri, Manchester United wamefufua malengo yao ya kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Sport, via Mail) Tottenham na Arsenal wameongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Brazil Willian kwa sababu mashauriano ya kiungo huyo wa miaka 31 kurefusha mkataba Chelsea yamegonga mwamba. (football.london) Ni vita ya fedha Tottenham dhidi ya Arsenal kuwania saini ya Willian, wengine sokoni Hamza Fumo 45 mins ago 35 Shanghai Shenhua inatarajia kuwa mshambuliaji wake Odion Ighalo, 30, raia wa Nigeria atarejea klabu hiyo baada ya kuchezea Manchester United kwa mkopo kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya

Zambia yatangaza kufunga mpaka wake na Tanzania kisa Corona

Image
Zambia imechukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufunga mpaka wake na nchi jirani ya Tanzania kuanzia Leo Jumatatu. Hii ni baada ya kuwa na maambukizi mengi, hususan miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwemnye miji ya mipaka nchini humo. Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuripoti wagonjwa 76 wa virusi vya corona katika mji uliopo katika mpake wake na Tanzania Kufikia sasa taifa hilo limethibitisha wagonjwa 367 wa virusi vya corona nchini humo. Akizungumza kwa niaba ya rais wa taifa hilo, Edgar Lungu Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alitangaza kwamba mpaka huo utafungwa kwa muda . Alisema kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo kuwekwa. Katika muda huo, amesema wafanyakazi wa uhamiaji katika mpaka huo watapatiwa mafunzo mapya ya jinsi ya kuhudumia mizigo na raia wanaoingia. ”Hali kule Nakonde ni mbaya na hii leo rais Edgar Lungu ana wasiwasi , Hivyobasi ameagiza kuanzia Jumatatu

Virusi vya corona: Obama asema hatua zilizochukuliwa na Trump ni kama 'janga la machafuko'

Image
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obam amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa namna anavyoshughulikia janga la corona. Kauli yake ameitoa alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wake wa zamani kuungana na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden, televisheni ya CNN imeeleza Ikulu ya Marekani imejibu kuwa hatua ya Rais "isiyo ya kawaida" ilikuwa "imeokoa maisha ya Wamarekani". Wakati wa simu hiyo, Bw Obama alisema mbinu ya mrithi wake wa Republican kwa serikali ni sehemu ya kulaumiwa kwa namna alivyolishughulikia janga la corona. Bwana Obama pia amekosoa vikali uamuzi wa kufuta mashtaka dhidi ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Michael Flynn. Hali ikoje nchini Marekani? Zaidi ya watu 77,000 wamepoteza maisha na Marekani sasa ina wagonjwa milioni 1.2 wa virusi vya corona, takwimu hizo zote ni za juu zaidi ulimwenguni. Nchi nyingi ziliweka marufuku ya kutotoka nje mwezi Machi, lakini masharti hayo sasa yameondolewa, na kuruhusu watu kurudi kwenye shughuli zao. Lakin

DAWA YA KORONA KUFIKA TANZANIA KUTOKA MADAGASCAR.

Image
Serikali ya Tanzania leo imepokea kutoka Serikali ya Madagascar msaada wa dawa zinazofubaza virusi vya corona. Ikumbukwe katika Hotuba ya Rais Magufuli siku tano zilizopita alisema kuwa . “Nimewasiliana na Madagascar kuna dawa ya corona wameipata nitatuma Ndege hiyo dawa ije hapa, tutumie dawa, tuombe Mungu bila kuchoka huu ugonjwa utaondoka tu” “Watanzania corona isitutishe, inawezekana kuna Watu wengine wamekufa kwasababu ya hofu tu, Viongozi wa Dini msitupotoshe, nampongeza Mufti amesema sisi tutaendelea kufunga, Watanzania tusimame imara tumeshashinda hii vita”

Profesa kutoka China aliyekuwa akifanya Utafiti kuhusu Corona Marekani auawa

Image
Mauaji ya raia wa China, mtafiti wa masuala ya virusi vya corona kwenye ardhi ya Marekani yamesababisha nadharia mbalimbali duaniani kuwa kuna sababu iliyojificha kuhusu kifo chake. Bing Liu, profesa msaidizi mwenye miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Pittsburgh, Marekani alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake siku ya Jumamosi. Wenzake walisema alikuwa karibu kupata “matokeo muhimu” ya tafiti kuhusu Covid-19, tukio lililosababisha kuwepo kwa maoni mitandaoni yanayoeleza kuwa yawezekana bwana Liu aliuawa lakini polisi wanasema ni tukio la kujiua. Kwa nini Liu aliuawa? Alikutwa akiwa na majeraha mengi ya risasi kichwani,shingoni katika eneo la Pittsburgh yalipo makazi yake kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo. Mtu aliyekuwa na silaha alitambulika kuwa na miaka 46, mhandisi wa programu ya kompyuta, Hao Gu. Mamlaka zinasema muuaji naye alijiua baada ya kurudi kwenye gari lake. Liu na Gu walikuwa wanafahamiana, maafisa wapelelezi wa mauaji walieleza. Uchunguzi umebaini kuwa lilikuwa tuki

TDiamond aanza kutimiza ahadi ya kuzilipia familia 500 kodi kwa miezi 3, Familia 57 zanufaika bado 443

Image
Msanii na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasafi, Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ ametoa msaada wa kodi ya pango kwa watu 57 ambao ni Wajane, Walemavu pamoja na Wasiojiweza. Msaada huo ni awamu ya kwanza katika dhamira yake ya kusaidia kodi ya pango kwa Kaya 500 nchini zilizoathirika kiuchumi na janga la #CoronaVirus. Diamond ametoa msaada huo siku ya Jumatatu ya tarehe 4/5/2020 katika Makao Makuu ya Kampuni ya WasafiMedia baada ya watu zaidi ya 100 kujitokeza ofisini hapo ambapo familia 57 zimeweza kupata msaada huo. Kwa Familia 443 zilizobaki bado mchakato unaendelea kwa ajili ya kuzipatia msaada huo.

Mwijaku: “Nyimbo za Diamond kuanza kuchezwa Clouds ataanza kushinda tuzo, Alipotea kimataifa”

Image
Msanii na Mtangazaji wa Cloud Plus @mwijaku ametoa maoni yake kuhusu CEO wa Clouds media @josephkusaga kuwataka Watangazaji wa kipindi cha Leo tena kucheza wimbo wowote wa @diamondplatnumz na @mwijaku kusema kwamba huo ndio Utakuwa mwanzo wa @diamondplatnumz kuanza kushinda tuzo. @mwijaku ameongeza kuwa @diamondplatnumz kutokushinda tuzo za kimataifa ni kwa sababu nyimbo zake ziliachwa kuchezwa Clouds media. Pia kwa Upande wa @lilommy alishinda tuzo kwa sababu baadhi ya Watangazaji wa Clouds walianza kumtaja kama @bdozen na wengine.