Nchi za Rwanda na Nigeria kuanzia leo Jumatatu zimeanza kulegeza masharti ya amri ya kusalia ndani kwa wananchi wake kama sehemu ya mapambano dhidi ya corona. Nchini Rwanda marufuku hiyo ilikuwa imewekwa nchi nzima, huku Nigeria marufuku hiyo ilihusisha ndani katika mji mkuu wa Abuja, na mji mkubwa kabisa wa Lagos, katika jaribio la kupunguza athari ya kiuchumi barani Afrika. Nchi hizo mbili, zinaungana na mataifa mengine ya Afrika kama Ghana, Afrika Kusini na Kenya ambayo pia yamelegeza baadhi ya masharti makali ya hatua hizo za watu kusalia ndani. Mataifa kadhaa ya Afrika yamechukua hatua ya kuweka marufuku hiyo toka mlipuko wa virusi hivyo kuingia barani na kuonesha hatari ya maambukizi ya ndani ya jamii. Uganda pia inatarajiwa kutangaza kulegeza masharti kesho. Raisi Museveni anatarajiwa kulihutubia taifa hilo jioni ya leo. Baadhi ya shughuli za kibiashara zinatarajiwa kufunguliwa japo shule zinatarajiwa kuendelea kufungwa mpaka hapo itakapotangazwa. Japo hatari ya virusi ingalipo,
Comments
Post a Comment