HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA
KUZALIWA Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 katika kijiji cha LUHOTA nje kidogo na mjini Iringa. Jina halisi aliitwa MKWAVA au MKWAVINYIKA likiwa na maana ya MTAWALA WA NCHI, Mkwawa alikuwa mtoto wa chifu aliyeitwa MUNYIGUMBA aliyekufa mwaka 1879. Baba yake alifanikiwa kuunganisha temi ndogondogo za wahe he na makabila ya jirani na kuwa dola moja , mfumo huo alinakili toka kwa falme za WASANGU waliowahi ku wa kabila lenye nguvu amabalo mbinu hii pia nao walijifunza toka kwa WANGONI. Hadi miaka ya 1870 eneo la wahehe lilipanuliwa kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo. Baada ya kifo cha chifu MUNYIGUMBA watoto wake waliingia tofauti kubwa sana katika harakati ya nani achukue madaraka ya hayati baba yao. mwi sho mkwawa alishinda na akawa kiongozi mpya wa wahehe Mkwawa aliendelea kupanua dola ya wahehe hadi kufikia mwaka 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na ziwa Tanganyika. Ambapo misafara hiyo ilikuwa ikibeba bidhaa za nje kama vita mbaa, visu, silaha kutoka pwani na ziwa Tanganyika. Misafara hiyo ilipaswa pia kulipa kodi iliyojulikana kama HONGO ambayo iliongezwa uwezo wake nguvu za kijeshi na kiutwala kwa ujumla MKWAWA NA UVAMIZI WA WAJERUMANI Tangu mwaka 1855 hivi, Wajerumani walianza kuunda Koloni lao katika Tanzania bara, Rwanda na Burundi ya leo. mnamo mwaka 1891 mkwawa alituma jeshi lake katika kambi ya WAJERUMANI iliyokuwepo mpwapwa na akawaadhibu vibaya wajerumani, sambamba na eneo la USAGARA ambako nako pia alishinda vita dhidi ya wajerumani. Gavana mpya wa kijerumani EMIL VON ZELEWSK alisikia habari za uvamizi wa wahehe, na akaomba kibali cha kuwashambulia wahehe toka BERLIN. EMIL VON ZELEWSK KIONGOZI WA WAJERUMANI ALIYEONGOZA VITA ZA LUGALO
MAPIGANO YA LUGALO Mwezi julai 1891 Von Zelewsk aliongoza kikosi cha maafisa 13 na askari waafrika kutoka sudani 320 pamoja na wapagazi 113. walikuwa na bunduki za kisasa na mizinga midogo. Zelewsk aliwadharau wahehe kama washe nzi ambao walikuwa na mikuki na pinde tu kwahiyo hakuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali. Tarehe 17 agost 1891 Zelewsk na jeshi lake walipita eneo la LUGALO km kadhaa toka Iringa mjini MKWAWA alikuwa aki msubiri akiwa na askari wapatao 3000, Mkwawa aliwashambuliwa wajerumani kwa kushtukiza na dakika kadha wajerumani wengi waliuawa akiwemo kiongozi wao ZELEWSK, wachache kati yao walikimbia ili kujiokoa nafsi zao. ASKARI WA KIHEHE WAKIWA TAYARI KWA VITA
Comments
Post a Comment