Hali mbaya ya hewa imeilazimu NASA kuahirisha safari

Hali mbaya ya hewa imeilazimu kampuni ya wanasayansi wa anga ya SpaceX kusitisha uzinduzi wa chombo cha Nasa astronauts Doug Hurley na Bob Behnken katika kituo cha anga cha kimataifa (ISS).
Wanaume hao wawili walikuwa wana nia ya kwenda kwenye kituo cha anga cha Kennedy ambapo inadaiwa kuwa jaribio la kwanza katika kituo cha anga ya juu kufanyika Marekani tangu miaka 9 iliyopita .

Lakini hali mbaya ya hewa ilisababisha waongozaji wa mitambo kusitisha uzinduzi huo, dakika 16 kabla ya roketi hizo kuanza safari.

Fursa nyingine ambayo SpaceX na Nasa wanayo ni kufanya jaribio jingine Jumamosi.

Na kama haitawezekana, watapata fursa nyingine Jumapili.

Changamoto ya hali ya hewa ilianza saa moja kabla ya muda wa uzinduzi kufika.

Lakini maamuzi ya kubadili uzinduzi yalikuwa ya ghafla wakati ambao roketi ya SpaceX Falcon na kikosi chake cha Dragon walikuwa wanapaswa kuondoka katika muda uliopangwa la sivyo wangeshindwa kufika katika muda kukipata kituo cha anga cha kisayansi.

Hii inamaanisha kuwa kila mmoja alipaswa kukaa chini akiwemo rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump, na waziri mkuu Mike Pence na mke wake Karen. Wote walifika kuangalia maadhimisho hayo ya kihistoria.
"Ninafahamu kuwa wamekatishwa tamaa leo. Hali ya hewa imetuangulisha," alisema kiongozi wa Nasa Jim Bridenstine. "lakini hii ilikuwa siku njema kwa Nasa na kwa SpaceX. vikosi vyetu vilifanya kazi kwa pamoja kwa weredi,na kufanya maamuzi sahihi wakati wote.

Hivyo tufanye hivyo tena , tufanye hivyo tena Jumamosi. Itakuwa siku nzuri sana."

Mpango huu una malengo mazuri, tangu kufungwa kwa safari hizo mwaka 2011, ambapo Marekani ilizindua chombo chake katika kituo cha anga - ni muda mrefu tangu Marekani itegemee vyombo vya Urusi.

Lakini dhamira ya Hurley na Behnken ilikuwa ni zaidi ya kupata umaarufu.

Nasa inaachana na shughuli zao za zamani za kumiliki na kushughulikia mifumo ya anga inayotaka kutumika katika mzunguko mdogo wa dunia katika siku za usoni kwa ajili ya kununua kikosi binafsi kwa ajili ya kununua huduma ya usafiri katika sekta binafsi- ni kama kampuni itahitaji vyanzo vya nje vya malipo na mahitaji muhimu.

SpaceX ni kampuni ya kwanza kutoa huduma mpya.

Bwana Bridenstine anaamini kuwa jitihada hizo zitasaidia kusaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika katika mpango wa mwezi na sayari ya Mars.

"Tumeangalia namna nzuri kwa ajili ya siku za usoni katika mzunguko mdogo wa dunia hivyo ni suala la kibiashara, Nasa ni mteja mmoja ambaye ana wateja wengi, tuna wasambazaji wengi ambao wamefika dau linaloshindaniwa, wana uvumbuzi mzuri na wanazingatia usalama," alisema.
"Tunatoa muundo wa kibiashara ambao utatoa mwanya wa kwenda katika mwezi,hii naona ni njia bora na kudumu. Kwa maneno mengine, tutaenda mwezini kukaa."

Jaribio la uzinduzi wa chombo cha anga lililokuwa lifanyike Jumatano huku kukiwa na janga la virusi vya corona.

Mkusanyiko wa watu ulitakiwa kukaa karibu na jukwaa la Kennedy complex, na Nasa yenyewe ilikaribisha idadi ndogo ya wageni katika eneo la tukio.

Wasafiri hao wa anga , wanapaswa kukaa karantini kabla ya kuanza safari ya angani. Lakini Nasa ilipunguza tena idadi ya watu ambao watakutana nao na walipewa muongozo wa kuvaa barakoa.

Fursa ya jaribio lingine litakuwa Jumamosi kama litafanyika litakuwa saa 15:22 EDT.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mchungaji Kyashama “Upinzani kazi yao kuiongelea vibaya Serikali wanatia aibu, Rais Magufuli anapewa maono na Mungu”