ZAWADI YA MAISHA

Ni tarehe 16 Novemba tena! Mvua zinanyesha kama ilivyokuwa katika siku kama hii miaka 45 iliyopita. Natamani ungekuwepo ili ushuhudie kinachoendelea sasa hivi katika kusanyiko hili kuu, lakini haiwezekani…. Haiwezekani Aurelia..!!!

Aureliaa….. mwanamke wa ndoto zangu, mwanamke uliyenitambulisha kwenye dunia ya mapenzi…nitawezaje kukusahau ewe muhebi wangu!

Nakumbuka tarehe kama hii mwaka ya 1968, ndiyo ilikuwa tarehe ambayo mimi na wewe tuliangukia penzini. Naikumbuka sana siku hiyo, ni siku ambayo nilikuwa natoka kuuza maziwa kwenye Senta ya kijiji chetu, mara ghafla mvua ikanikutia njiani kabla sijafika 
nyumbani kwetu, nikaja kujibanza upenuni mwa
nyumba yenu ili kujikinga nisilowe. Hapo nikakutana na wewe ukiwa unakinga maji ya mvua ile, kutokana na kunyeshewa sana… gauni lako lililowa na kushikamana na mwili wako na kuyafanya maungo yako yajichore juu ya gauni lile. Chuchu zako za saa sita zilizochongoka mithili ya miba, zilikuwa kama vile zinang’ang’ana kutoboa gauni lako bila mafanikio, ndiyo zilinifanya nikapagawa sana kiasi cha kushindwa kutambua kama nilikupenda, au nilikutamani kwa wakati ule!

Wakati bado natafakari cha kufanya mara ghafla... nikashituliwa na sauti yako, ukiomba nikutwishe ndoo ya maji. Siyo siri Aurelia, nilitamani kukimbia kwa sababu ya uyabisi uliokuwa umejiunda kwenye tupu yangu ya mbele, uyabisi uliokuja baada ya kuyaona maungo yako ya ndani yaliyokuwa yamejichora juu ya gauni lako. Moyoni nilipatwa na aibu isiyo kifani, lakini bado niliisikia sauti yako ukinisihi nikutwishe.

Huku nikiwa nimejawa na aibu, niliinama nikaishika ndoo, nawe ukaishika, kwa pamoja tukainyanyua juu na kuiweka kichwani kwako huku nyuso zetu zikiwa zimekaribiana!Nikiwa bado nimejawa na aibu kiasi cha kushindwa hata kukutazama, nikashituliwa tena na sauti yako ukisema, “Usiondoke nisubiri” nikahisi kupagawa tena!

Auerelia ukaondoka na ndoo yako ya maji kichwani, mara punde ulirudi, ukanishika mkono na kuniongoza kwenye jumba lisiloisha, ambalo lilikuwa pembeni ya nyumba yenu, tukafanya mapenzi kwenye mvua, mapenzi yaliyonifanya niipate raha ya ajabu, raha ambayo sikuwahi kuipata kabla!

Siku hiyo tuliagana tukiwa na furaha, huku ukiniahidi kuwa ni lazima unipe zawadi ambayo itanifanya nikukumbuke siku zote za maisha yangu, ‘Zawadi ya Maisha’, huo ukawa ukurasa wa kwanza!

Hamu ya kutaka kuwa karibu na wewe kila mara ilinifanya nipate wakati mgumu sana… pale ambapo siku iliisha bila kukutia machoni, siyo kama siku haikuisha.. la hasha! Siku iliisha, lakini iliisha kwa tabu sana.

Tukaendelea na mapenzi yetu kwa raha mustarehe kama wa hadithini japo kwa kificho, mpaka pale ulipokuja kushika mimba, mimba ambayo ilitufanya tuwe wakimbizi baada ya wewe kufukuzwa kwenu huku baba yako akiapa kuniua endapo angenikamata.Bado sijasahau Aurelia, tuliishi maisha ya shida ukimbizini huku mimba yako ikizidi kukua siku hadi siku, mpaka ilipofika tena tarehe 16 Novemba ya mwaka 1969, mpenzi wangu ukajifungua mtoto wa kiume chini ya mti.. mimi nikiwa kama mkunga!

Furaha yangu ikadumu kwa muda mfupi, kabla haijayeyuka kama pande la barafu kwenye jua kali, kwani ulivuja damu nyingi hadi ukadhoofu, lakini kwa tabu ulifungua kinywa ukasema, “hiyo ndiyo zawadi niliyokuahidi, zawadi ya maisha… nakuomba uitazame kwa macho mawili na uikumbatie kwa mikono miwili… jina lake ni IMORI….jina la marehemu babu yako” Mpenzi hukuendelea zaidi ukaiaga dunia mbele yangu na mwanetu ambaye ghafla alianza kulia, nami nikajumuika naye katika kulia, ukawa umetutoka!

Nilichimba kaburi nikiwa peke yangu, huku mvua ikiwa inanyesha, nikakuhifadhi na juu yake nikaweka msalaba, tukaondoka tukakuacha peke yako porini ukiwa umelaliwa na lundo lile la udongo, mpaka miaka mitano baadaye niliporudi na mwanetu kipenzi kuja kumuonesha ulipolala mpendwa wetu…, Mungu akulaze mahala pema peponi Aurelia.
Leo tena ni tarehe 16 Novemba ya mwaka 2013, miaka 45 tangu tulipo kutana kwa mara ya kwanza, na miaka 44 tangu uage dunia mbele ya macho yangu na mwanao. Tuko hapa leo kwenye kusanyiko kuu, nikiwa na wajukuu zako, Pendo, Furaha na Aurelia mrithi wa jina lako, tuko pamoja na wananchi wengine kwenye kusanyiko hili kuu tukimshuhudia mwanao kipenzi ‘IMORI’ akiapishwa kuwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, raisi aliyechaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi wa huru na wa haki, Ubarikiwe Aurelia mzaa chema!

Aurelia mwanamke wa maisha yangu, mwanamke wa ndoto zangu uliyenipa zawadi ya maisha, mizinga hii 21 anayopigiwa mwanao kwa heshima leo hii, ni kwa ajili yako na mvua hizi zinazoendelea kunyesha katika tarehe hii, tarehe ambayo inanikumbusha mengi katika maisha, zinyeshee mbegu za upendo uliokuwa nao ili uzidi kuchipuka kwa mwanao na wanae na hatimaye usambae kwa watanzania wote ili wawe upendo uliokuwa nao ili uzidi kuchipuka kwa mwanao na wanae na hatimaye usambae kwa watanzania wote ili wawe na mapenzi mema kwa nchi yao na rasilimali zake, ili wote tujumuike kuifurahia zawadi hii, zawadi ya maisha!

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho