Kifo cha George Floyd: Maandamano yatanda kote Marekani kudai haki

Waandamanaji wakusanyika nje ya Ikulu pamoja na maeneo mengine juu ya kifo cha raia mweusi George Floyd.


Waandamanaji wanakabiliana na polisi katika miji mbalimbali nchini Marekani juu ya mauaji ya raia mweusi wa Marekani ambaye hakuwa na silaha aliyekufa mikononi mwa polisi huko Minneapolis.

Gavana wa Minnesota amesema kwamba kifo cha George Floyd aliyekuwa kizuizini kimeonesha mauaji ya kiholela.

New York, Atlanta na maeneo mengine yamekuwa yakishuhudia ghasia huku Ikulu ya Marekani ikiwekewa katika hatua ya kusalia ndani kwa muda mfupi.

Aliyekuwa afisa wa polisi katika eneo la Minneapolis ameshtakiwa kwa mauaji kutokana na kifo hicho.
 
 Hali ilivyo hadi kufikia sasa?

Katika mji wa New York, eneo la Brooklyn, waandamanaji walikabiliana na polisi kwa kuwarushia chochote walichoona, kuwasha moto na kuchoma moto magari ya polisi.

Maafisa kadhaa wa polisi walijeruhiwa.

Mayor Bill de Blasio aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter: "Hatutaki kushuhudia usiku mwengine kama huu."

Tayari raia walikuwa na hasira juu ya kuuawa kwa raia wengine wawili weusi, Ahmaud Arbery mji wa Georgia na Breonna Taylor.

Polisi anayehusishwa na mauaji ya George Floyd ameshtakiwa
Aliyekuwa afisa wa Minneapolis amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya mauaji baada ya kutokea kwa kifo cha mwanamume mweusi ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa kizuizini.


Derek Chauvin, ambaye ni mzungu, alioneshwa kwenye video akipiga magoti juu ya shingo ya George Floyd mwenye umri wa miaka 46, Jumatatu. Yeye pamoja na maafisa wengine watatu wamekamatwa.

Maandamano ya siku kadhaa katika mji wa Minnesota yamesababisha uharibufu wa mali na kuchoma moto majumba ambayo pia yamesambaa katika maeneo mengine nchini Marekani.

Tukio hilo limesababisha hasira na ghadhabu nchini humo juu ya matukio mengine kama hayo ambapo polisi huwaua raia weusi wasiokuwa na hatia.Mwendesha mashtaka alisema nini?
Mwendesha mashtaka Mike Freeman wa kaunti ya Hennepin alisema Bwana Chauvin alishtakiwa kwa makosa ya mauaji kiwango cha tatu huku kiwango cha pili kikiwa ni kuua bila kukusudia,

Aliongeza kuwa anatarajia kwamba wale maafisa wengine watatu pia nao watafunguliwa mashtaka lakini hakutoa maelezo zaidi.

Bwana Freeman alisema kuwa ofisi yake itaendesha kesi hii mara moja punde tu baada ya wao kupokea ushahidi".

"Hatujawahi kufungua mashtaka kwa haraka kiasi hiki dhidi ya afisa wa polisi," alisema.

Kwa mujibu wa aliye mshitaki kwa makosa ya uhalifu, Bwana Chauvin alichukua hatua akiwa na nia ya kushambulia bila kuzingatia ubinadamu.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho