Mfahamu Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye anatoka Chama cha Mapinduzi, kitaaluma ni mwalimu na mtalaamu wa kemia.
Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi huko huko Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1975 na baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza mwaka 1977 hadi 1978.

Kiongozi huyo alijiunga na chuo cha ualimu cha Mkwawa kilichoko Iringa, Kusini mashariki mwa Tanzania kati ya mwaka 1979 na 1982 ambapo alitunukiwa Stahahada ya Ualimu.

Baada ya kufuzu, alifundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbalimbali za sekondari kuanzia mwaka 1983.

Magufuli hakuishia hapo kielemu kwani aliamua kujiendeleza zaidi na kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 hadi 1988 ambapo alitunukiwa shahada ya ualimu katika masomo ya kemia na hisabati.

Baadaye, aliamua kukolea katika kemia na akarejea chuoni na kusoma hadi ngazi ya udaktari.

Siasa za Tanzania
Katika siasa, Magufuli mwanzoni hakujulikana sana hadi nyota yake ya kisiasa ilipoanza kung'aa pale alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995.

Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na baadaye akapanda ngazi hadi kuwa waziri kamili, nafasi aliyoishikilia hadi hivi sasa.

Kwa mujibu wa majirani wanaoishi karibu na nyumba yake jijini Dar es Salaam, yeye ni mtu anayeishi maisha ya kawaida.

Wakati watoto wa baadhi ya viongozi wakisoma shule za hali ya juu watoto wake wamesoma katika shule za kawaida.

Alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25, 2015, mpinzani wake mkuu akiwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa wa chama cha Chadema chini ya muungano wa Ukawa, na akaapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Novemba 5, 2015.


Elimu
2006 – 2009: PhD (Kemia ); Chuo Kikuu cha Dar es salaam

1991 – 1994: Msc. (Kemia); Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

1985 – 1988: Shahada ya kwanza katika Ualimu (Kemia na Hisabati);Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

1981 – 1982: Diploma ya Ualimu masomo ya Sayansi; Chuo cha Ualimu cha Mkwawa Masomo makuu Kemia, Hisabati na Ualimu.

1979 – 1981: Kidato cha tano na sita, Shule ya Upili ya Mkwawa, Iringa

1977 - 1978: Elimu ya sekondari, Shule ya upili ya Lake, Mwanza

1975 – 1977: Katoke Seminary, Biharamulo, Kagera

1967 – 1974: Shule ya Msingi, Shule ya Msingi Chato - Kagera

Mafunzo ya kijeshi
Machi 1984 – Juni 1984: Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa – Dodoma

Januari 1984 – Machi 1984: Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni– Arusha

Julai 1983 – Desemba 1983: Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora – Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho