Virusi vya corona: Obama asema hatua zilizochukuliwa na Trump ni kama 'janga la machafuko'

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obam amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa namna anavyoshughulikia janga la corona.

Kauli yake ameitoa alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wake wa zamani kuungana na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden, televisheni ya CNN imeeleza

Ikulu ya Marekani imejibu kuwa hatua ya Rais "isiyo ya kawaida" ilikuwa "imeokoa maisha ya Wamarekani".
Wakati wa simu hiyo, Bw Obama alisema mbinu ya mrithi wake wa Republican kwa serikali ni sehemu ya kulaumiwa kwa namna alivyolishughulikia janga la corona.

Bwana Obama pia amekosoa vikali uamuzi wa kufuta mashtaka dhidi ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Michael Flynn.

Hali ikoje nchini Marekani?
Zaidi ya watu 77,000 wamepoteza maisha na Marekani sasa ina wagonjwa milioni 1.2 wa virusi vya corona, takwimu hizo zote ni za juu zaidi ulimwenguni.

Nchi nyingi ziliweka marufuku ya kutotoka nje mwezi Machi, lakini masharti hayo sasa yameondolewa, na kuruhusu watu kurudi kwenye shughuli zao.

Lakini maafisa wa afya wanaonya kuwa hatua hii inaweza kusababisha virusi kusambaa zaidi.
Jitihada za Trump katika kupambana na virusi zimekuwa za nenda rudi.

Mwezi Februari alisema ugonjwa huu utatoweka , akitaka watu kuondokana na hofu lakini katikati ya mwezi Machi alieleza kuwa ugonjwa wa corona umekuwa ukisambaa kwa kasi nchini Marekani

Mwezi Aprili alipendekeza kuwa dawa za kuua bakteria zinaweza kuzuia virusi-jambo ambalo wanasayansi walilikana .

Juma lililopita alitangaza kuwa atavunja kikosi kazi kinachofanya kazi ya kupambana na virusi vya corona, lakini baadae alisema wataendelea na kazi -lakini akielekeza kufungua uchumi wa nchi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho