HISTORIA YA BENJAMINI MKAPA.
Benjamin William mkapa, alizaliwa 1938,ana watoto 2,
Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere. Na Chuo Kikuu cha Columbia Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu.
Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.
Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kwa kumuunga mkono kwa nguvu rais wa zamani Julius Nyerere
Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi,Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005.
Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na akaweka sera za soko huru.
Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.
Baada ya kutoka ofisini kutokana na kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa,
Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.
Mkapa aliitawala Tanzania kwanzia mwaka 1995 mwezi wa kumi tarehe 23 hadi 21/12/2005 ambapo alimwachia raisi aliemtangulia ambae ni Jakaya Kikwete, na aliemtangulia ni raisi Ali Hassan Mwinyi maarufu kama Ruksa.
Makamo wake wa raisi wa kwanza ni Omar Ali Juma (1995–2001) na alipokelewa na Ali Mohamed Shein (2001-05) ambae hivi sasa ni raisi wa Zanzibar na chama chake cha kisiasa ni CCM.
Mbali na hayo aliwahi pia kuwa waziri wa habari na utangazaji mwaka 1990 – 1992. Mkapa alizaliwa 11/ 1938 Eneo alililo zaliwa ni Ndanda, Masasi, hapa Tanzania.
Mh.Mkapa alimuoa mama wa kabila la kichaga aitwae Anna Mkapa na amefanikiwa kupata watoto wawili.
Kwa upande wa fani mkapa ni mwandishi wahabari na mwanadiplomasia.
Licha ya wasifu wake pia Benjamin William Mkapa, anazo sifa zake. Inasemekana ni rais aliyekuwa na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha juu ya jambo lolote lililoelekezwa kwake likihitaji ufafanuzi.
Wapo wanaosema kwamba hiyo inachangiwa na uwezo wa kiakili alio nao rais huyo mstaafu, lakini wengine wanasema hicho ni kipaji cha mtu wala hakina uhusiano na uwezo wa kiakili.
Lakini hata hivyo baadhi ya watu waliosoma na Mkapa katika sehemu mbalimbali, kuanzia shule za chini, shule za kati, St. Francis Pugu na hata Chuo Kikuu Makerere, wanasema Mkapa alikuwa na uwezo mkubwa darasani, vilevile uwezo mzuri wa kujieleza na kuitetea hoja yake hasa wakati wa midahalo.
Wanasema ni uwezo huo uliomfanya arushwe madarasa. Inasemekana sekondari aliisoma kwa miaka mitatu badala ya minne, na wengine wanasema kwamba shahada nayo aliisoma kwa miaka miwili badala ya mitatu, kama si kutia chumvi.
Pengine ni ukweli huo uliomshawishi Baba wa Taifa, ambaye kipindi fulani alikuwa mwalimu wake Mkapa, amwekee kifua ili aweze kuupata urais wa Tanzania.
Mwalimu alikuwa anaonyesha bila kificho jinsi alivyomuamini Mkapa. Na alikuwa anaonyesha uhakika kwamba Mkapa angeweza.
Comments
Post a Comment