Simba yafungua website yao rasmi, Manara na Senzo wafunguka wachezaji waliosajili pia mazoezi ya timu kuanza rasmi siku hii

Akiongea C.E.O wa klabu hiyo @football_senzo pamoja na msemaji wa klabu hiyo @hajismanara wametolea ufafanuzi juu ya Website hiyo ya Simba ambayo utakuta historia ya klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na Matokeo I ya michezo yote ambayo Simba imewahi kucheza, kwa maana nyingine taarifa zote za klabu hiyo tena kwa lugha mbili KISWAHILI na KIINGEREZA.
Mbali na hilo C.E.O bwana @football_senzo amesema kuwa kuna taarifa nyingi sana na amekuwa akipokea simu nyingi za mawakala kuhusu usajili mpya na kusema kuwa lengo lao kwa sasa ni kupeleka nguvu zao kwenye ligi wahakikishe wanashinda taji hilo kwani wapo kileleni mwa ligi lakini pia kupelekea macho na nguvu zao kwenye ligi ya AZAM FEDERATION na kuhakikisha wanafanya vizuri na baada ya hayo yote basi taarifa na wachezaji waliosajili watatangazwa rasmi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho