Ajuza wa miaka 103 apona Virusi vya Corona, ajipongeza kwa bia baridi



Ajuza mweye umri wa miaka 103, Jennie Stejna amejipongeza kwa kunywa bia ya baridi aina ya Bud Light, baada ya kupona ugonjwa wa Virusi vya Corona.


Bibi huyo anayepatikana Massachusetts Jijini Boston, alianza kuumwa ugonjwa huo mwanzoni mwa mwezi Mei, kwa dalili za kukosa ladha pia na kuumwa na homa kisha kupelekwa hospitali.


Kwa mujibu wa TMZ, Daily Mail na vyombo vingine vya habari, Akitoa taarifa hiyo mkwe wa mjukuu wake Adam Gunn amesema, wote walikuwa wanajua tayari wanaelekea kumpoteza bibi yao, na kuna siku aliwahi kumuuliza kama yupo tayari kwenda mbinguni kisha bibi akamjibu ndiyo.Mzee huyo kwa sasa ni mjane na mumewe alifariki mwaka 1992 akiwa na miaka 82, amebahatika kupata watoto wawili, wajukuu watatu, vitukuu wanne na vilembwekezi wanne.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho