Shule ya sekondari yapewa jina la Jokate Mwegelo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ambayo inajengwa na kampeni ya Tokomeza Zero kupitia Harambee ambayo iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam na DC Jokate baada Jumamosi hii kutembelea na kujionea kazi kubwa iliyofanyika katika shule hiyo aliyoipa jina la Jokate Girls High School iliyopo Mhaga wilayani Kisarawe. .
Waziri baada ya kuona ujenzi huo ambao umekamilika kwa asilimia 70, alimpongeza DC Jokate huku akidai ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kubwa nchini Tanzania.
Pia alimtaka Mkurugenzi wa Kisarawe, shule hiyo ambayo mpaka sasa ina madarasa nane ya kisasa, maabara moja, bweni moja la wanafunzi 100 pamoja na nyumba moja ya mwalimu kuipa jina la Jokate Girl Secondary kutokana kazi kubwa iliyofanya na mkuu huyo wa wilaya.
Comments
Post a Comment