Corona: Hauwezi kukimbia kifo, baa, hotel na biashara zote zifunguliwe – RC Makonda
RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.
Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.
“Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea, Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwaiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida” Alisema RC Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelea kuchukuwa tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.
Comments
Post a Comment