Posts

Showing posts from April, 2020

Lukamba: “Diamond ni hatari kwa kujifukiza, Mama yake ndio fundi tunaenda mmoja mmoja tusiambukizane Corona”

Image
Mpiga picha wa msanii wa Bongo Fleva @diamondplatnumz @lukambaofficial ameeleza jinsi Boss wake @diamondplatnumz anavyojifukiza kwa lengo la kujikinga na Corona. Lukamba ameongeza kuwa @diamondplatnumz ni hatari sana kwa kujifukiza maana @mama_dangote ndio fundi wa mambo hayo “Tunajipiga nyungu mmoja mmoja kuhofia kuambukizana Corona.

RC Makonda atoa msaada wa mabati yenye gharama ya mil 476 kuhudumia nyumba 1000

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane, mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka. RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko. na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani* baada ya kukosa makazi ya kuishi* hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya *pole kwa adha waliyoipata.* Aidha *RC Makonda* amewapa *siku 10 Wakuu wa Wilaya* kuhakikisha *wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.* Aidha *RC Makonda* amesema *athari zinazoonekan

Mfahamu Irrfan Khan, Mcheza filamu maarufu India aliyepoteza maisha

Image
Muigizaji huyo maarufu kutoka tasnia ya filamu za Kihindi (Bollywood) aliyetamba katika filamu za ‘Slumdog Millionaire’ na ‘Jurassic World’ amefariki leo asubuhi akiwa na miaka 53. Mwaka 2018, alitangaza kuwa na saratani katika mfumo wa tezi zinazotengeneza homoni (Endocrine Tumour). Tangu jana amekuwa kwenye Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) hospitali kutokana na bakteria kwenye utumbo ‘Colon Infection’. Mwaka 2013, alishinda tuzo ya Kitaifa ya Filamu za India kutokana na filamu ya Paan Singh Tomar. Filamu nyingine alizotamba nazo ni Lunchbox, The Namesake, New York, I Love You na Hindi Medium. Ya mwisho, Angrezi Medium imetoka mwezi uliopita. Khan amezikwa katika makaburi ya Versova Kabristan huko Mumbai muda mfupi baada ya taarifa zake za kifo kutolewa. Familia, ndugu na marafiki wa karibu ndio wamehudhuria.

Waziri Mkuu ” Waliopona Corona Tanzania wafika 167 Bara 83 na Visiwani 36, Vifo 16″

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini ambapo amesema kuwa kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480. Aidha Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83). Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa. Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila Kifo kinachotokea hakisababishwi na Ugonjwa wa Corona.

Diamond aonyesha hoteli aliyoinunua na kuamua kuitoa itumike kama karantini ya watu wenye Corona.

Image
Diamond amesema kuwa “Nimenunua Hotel maeneo ya mikocheni, nimeshakabidhiwa documents zangu , ipo kwenye marekebisho kadhaa Kisha nitaitambulisha” Hotel niliyonunua kwasababu sijaanza kui upgrade , Niko radhi niitoe kwa serikali kwa muda huu ili iweze kutumika Kama Karantini au Hospitali mpaka pale Corona itakapoisha”

WEMA WA MSHUMAA.

Image
Wahenga wanasema tenda wema nenda           zako,hii inaleta maana kuwa si kila unapotenda wema kwa mtu basi usibiri kushukuriwa. Wapo watu wa aina tofauti tofauti tunao ishi nao katika jamii zetu,na kila mtu ana tabia yake, Alikuwepo kijana mmoja ambae kazi yake ni kuwahudumia wanyama,hasa yeye alihusika sana na kuwahudumia simba, Aliwalea tangia wakiwa wadogo mpaka wanakua simba hao. Aliwapa chakula cha kutosha,na kuwapa dawa hasa pale wanapo onesha dalili za kuumwa,pia maji ya kutosha,na aliwapenda sana hao simba mpk kuwasafishia ata katika banda walimokuwa wanalala.  Lakini siku moja huyo kijana wakati akiwasafishia lile banda aliwaamisha na kuwafungulia sehemu nyingine waingie ili aweze kusafisha,lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufunga kwa kukaza lile banda. Simba waliugonga mlango na kuingia ndani alimokuwa yule kijana na kuamshambulia vibaya mpaka kupelekea kufariki kwa yule muhudumu. Mwisho walikuja walinzi waliosikia kelele alizokuwa akipiga yule kijana,na kuwashambulia wale

Haji Manara atoa ya moyoni baada ya Diamond kutangaza kulipia familia 500 kodi “Wapo wabishi watasema kwanini umetangaza”

Image
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram baada yaDiamond kutangaza kulipia familia 500 kodi za nyumba kwa miezi mitatu. Haji Manara alichukua ujumbe aliopost Diamond na kuupost kwenye ukurasa wake wa Instgram na kuandika maneno haya: “Sijawahi kujuta kuwa na ushkaji na ww,,wapo wabishi watasema mbona umetangaza? Ahhhh !! Hii ni kwa ajili ya kuwainspire wengine waliojaaliwa kdogo kuwatazama wenzao!! Unajua nn Mwamba? Mungu atakuongezea ile mbaya,,atakufungulia Rizk zaidi na kwa sasa bado kitu kimoja tu ,,ukifanya hvyo na Peponi tutakaa Wote Inshaallah,,,,.. OA @diamondplatnumz“

Diamond atangaza kuzilipia kodi familia 500 zilizoathirika na Corona kwa miezi mitatu kila familia

Image
Msanii wa mizki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametangaza kuwalipia kodi watu 500 walioathirika na Corona kwa miezi mitatu kila mmoja. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika ujumbe huu. “Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara….nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba…. #HiliNaloLitapita #ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona.

Waislamu waanza mfungo wa mwezi wa Ramadhan

Image
Waislamu kote ulimwenguni wanaanza ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, katikati ya sintofahamu inayotokana na hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona ambazo ni Pamoja na kuwazuia watu kutoka nje. Waislam waanza mfungo wa mwezi wa Ramadhan Virusi vya corona kwa kiasi kikubwa vimebadilisha mfumo wa Maisha duniani, huku mataifa yakipambana kwa kila hali kukabiliana na maradhi yanayosababishwa na virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19. Karibu vifo 190,000 vimetokea kutokana na ugonjwa huo, idadi ya walioambukizwa hivi sasa inakaribia milioni 2.7, na pia uchumi wa dunia umeathirika pakubwa. Waumini wa dini ya Kiislamu kuanzia Kusini Mashariki mwa Asia hadi Mashariki ya Kati na hata Afrika wanaanza mwezi huu mtukufu katikati kadhia ya mapambano haya, kwa kuzuiwa kukusanyika na hata kutoka nje. Hawaruhusiwi kukusanyika kwa ibada misikitini na hata kufanya mikusanyiko mikubwa ya kifamilia pamoja na marafiki wakati wa futari nyakati za jioni baada ya siku nzim

Wanasayansi Uingereza wataka chanjo yao ya Corona kufanyiwa majaribio Kenya

Image
Watafiti kutoka nchini Uingereza wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya ambapo kulingana na wao mlipuko wa ugonjwa huo unaongezeka.          Hatua hiyo inajiri siku cha tu baada ya Shirika la Afya duniani kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo. Mkuu wa Shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za “kibaguzi” kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika. “Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus. Mkuu wa shirika la Afya Duniani Dkt Tedros Adhanom Ghebreyes amesema kwamba bara la Afrika halitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo ya corona Kwa mujibu wa Citizen ya Kenya ,BBC, Daily Monitor na vyombo vingine vya habari, Hata hivyo wanasayansi hao kutoka Chuo kikuu cha Oxford wanadaiwa kufikiria wazo hilo iwapo hawatopata matokeo ya hara

Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa

Image
Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa Ally Juma 45 mins ago 87 Dawa iliyokuwa ikitazamiwa kutibu virusi vya corona inaripotiwa kushindwa kufikia viwango vya ufanisi katika jaribio la kwanza la matibabu. Kumekuwa na matumaini makubwa kwamba dawa ya remdesivir ingeweza kutibu ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19. Lakini jaribio la dawa hiyo nchini Uchina limeonesha kuwa dawa hiyo haikufanikiwa, kwa mujibu wa waraka uliochapishwa kimakosa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Dawa hiyo haikuboresha hali za wagonjwa au kupunguza kiwango cha virusi katika damu, ulisema waraka huo. Kampuni ya Marekani inayotengeneza dawa hiyo, Gilead Sciences, imesema kuwa waraka huo ulipotosha uchunguzi wake. Kipi tunachokifahamu kuhusu utafiti huo? Taarifa juu ya kushindwa kwa jaribio la dawa hiyo ilisambaa baada ya WHO kutuma maelezo katika kanzidata (hofadhi ya kumbuk

Mchungaji Dkt Getrude Rwakatare azikwa leo kanisani kwake (+Picha)

Image
Mwili wa Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Dkt Getrude Rwakatare umezikwa leo kanisani kwake huku ibada ya mazishi ikihudhuriwa na idadi ndogo ya watu kama ilivyoelekezwa na serikali. Maziko ya Askofu Getrude Rwakatare yafanyika katika eneo la Kanisa la Mlima wa Moto lililoko Mikocheni B, Jijini Dar Es Salaam. Mchungaji huyo wa Kanisa la Mlima wa Moto na Mbunge wa viti maalum CCM, Askofu Gertrude Rwakatare alifariki Dunia alfajiri ya April 20, 2020, Maziko ya Askofu Getrude Rwakatare yafanyika katika eneo la Kanisa la Mlima wa Moto lililoko Mikocheni B, Jijini Dar Es Salaam. Mchungaji huyo wa Kanisa la Mlima wa Moto na Mbunge wa viti maalum CCM, Askofu Gertrude Rwakatare alifariki Dunia alfajiri ya April 20, 2020,

HALLOW

Image
kingShyzzoh