Wanasayansi Uingereza wataka chanjo yao ya Corona kufanyiwa majaribio Kenya

Watafiti kutoka nchini Uingereza wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya ambapo kulingana na wao mlipuko wa ugonjwa huo unaongezeka.
        
Hatua hiyo inajiri siku cha tu baada ya Shirika la Afya duniani kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo.

Mkuu wa Shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za “kibaguzi” kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

“Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Mkuu wa shirika la Afya Duniani Dkt Tedros Adhanom Ghebreyes amesema kwamba bara la Afrika halitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo ya corona

Kwa mujibu wa Citizen ya Kenya ,BBC, Daily Monitor na vyombo vingine vya habari, Hata hivyo wanasayansi hao kutoka Chuo kikuu cha Oxford wanadaiwa kufikiria wazo hilo iwapo hawatopata matokeo ya haraka nchini Uingereza.

Chanjo hiyo inajulikana kutoa antobody yenye nguvu, lakini hilo halimaanishi kwamba inaweza kuwa kinga.

”Tutalazimika kuhitaji chanjo chungu nzima , kuna nyingi zinazofanyiwa majaribio hivyo basi tutahitaji dozi nyingi na tutarajie mjadala mkubwa kuhusu ni mataifa gani ama ni kundi lipi la watu linalohitaji chanjo hiyo kwanza”, alisema mwandishi wa BBC wa maswala ya tiba Fergus Walsh.

Alikuwa akizungumza katika runinga ya BBC News ambapo mtangazaji Sophie Raworth alimtaka kutoa mtazamo wake kuhusu ufanisi wa chanjo hiyo.

Walsh alijibu akisema kuna umuhimu kuwa makini na ahadi zinazotolewa kutokana na kile alichokitaja kuwa hamu ya chanjo hiyo kufanya kazi.
Idadi ya wanaoshiriki katika utafiti huo
Watu wawili waliojitolea , wote wakiwa wanasayansi walichomwa sindano ya chanjo na ndio watu wa kwanza kati ya zaidi ya watu 800 walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 55 ambao walichaguliwa kufanyiwa utafiti huo.

Mtu wa kwanza kujitolea alitambulika kuwa mwanasayansi kwa jina Elisa Granato aliye katika idara ya wanyama katika chuo kikuu cha Oxford.

”Mimi ni mwanasayansi na nataka kusaidia sayansi, kwa uwezo wangu wote na kwasababu sifanyi utafiti wa virusi, nilihisi hii ndio jinsi ninavyoweza kusaidia katika utafiti huu. Ndio maana niko hapa na nafurahia”, alimwambia Walsh.

Nusu ya kundi hilo litapokea chanjo ya Covid 19 huku nusu nynegine ikipokea chanjo ya udhibiti ambayo inalinda dhidi ya ugonjwa wa menenitis lakini matokeo yake hayatajulikana kwa miezi kadhaa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho