HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA
KUZALIWA Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 katika kijiji cha LUHOTA nje kidogo na mjini Iringa. Jina halisi aliitwa MKWAVA au MKWAVINYIKA likiwa na maana ya MTAWALA WA NCHI, Mkwawa alikuwa mtoto wa chifu aliyeitwa MUNYIGUMBA aliyekufa mwaka 1879. Baba yake alifanikiwa kuunganisha temi ndogondogo za wahe he na makabila ya jirani na kuwa dola moja , mfumo huo alinakili toka kwa falme za WASANGU waliowahi ku wa kabila lenye nguvu amabalo mbinu hii pia nao walijifunza toka kwa WANGONI. Hadi miaka ya 1870 eneo la wahehe lilipanuliwa kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo. Baada ya kifo cha chifu MUNYIGUMBA watoto wake waliingia tofauti kubwa sana katika harakati ya nani achukue madaraka ya hayati baba yao. mwi sho mkwawa alishinda na akawa kiongozi mpya wa wahehe Mkwawa aliendelea kupanua dola ya wahehe hadi kufikia mwaka 1880 alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati ya pwani na ziwa Tanganyika. Ambapo misafara hiyo ilikuwa ikibeba bidhaa za nje kama vita mbaa, visu, silaha
mambo moto🔥🔥🔥🔥
ReplyDelete