RC Makonda atoa msaada wa mabati yenye gharama ya mil 476 kuhudumia nyumba 1000

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane, mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka.
RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko. na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani* baada ya kukosa makazi ya kuishi* hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya *pole kwa adha waliyoipata.* Aidha *RC Makonda* amewapa *siku 10 Wakuu wa Wilaya* kuhakikisha *wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.* Aidha *RC Makonda* amesema *athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji* jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka *kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.* Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema kwa sasa *serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko* ikiwemo ujenzi wa *madaraja ya muda mfupi* ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea. *RC Makonda* pia amewaelekeza *wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili wabuni design mpya zinazokidhi viwango.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho