Waziri Mkuu ” Waliopona Corona Tanzania wafika 167 Bara 83 na Visiwani 36, Vifo 16″

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya mwenendo wa Ugonjwa wa Corona nchini ambapo amesema kuwa kuna maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa watanzania 196 ambapo kati yao; kutoka Bara ni 174, Zanzibar 22 na kufanya jumla ya watu waliopata maambukizi kuwa ni 480.
Aidha Waziri Majaliwa amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, (Zanzibar wako 36, Bara ni 83). Hali kadhalika vifo 6 vimetokea na kufanya jumla ya waliofariki kwa ugonjwa wa Corona kufikia 16 hadi sasa. Waziri Mkuu ametoa rai kwa Watanzania kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila Kifo kinachotokea hakisababishwi na Ugonjwa wa Corona.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mchungaji Kyashama “Upinzani kazi yao kuiongelea vibaya Serikali wanatia aibu, Rais Magufuli anapewa maono na Mungu”