Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa


Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa
Jaribio la kwanza la dawa iliyotizamiwa kutibu Corona lashindikana, Sababu hizi zaelezwa
Ally Juma 45 mins ago 87




Dawa iliyokuwa ikitazamiwa kutibu virusi vya corona inaripotiwa kushindwa kufikia viwango vya ufanisi katika jaribio la kwanza la matibabu.



Kumekuwa na matumaini makubwa kwamba dawa ya remdesivir ingeweza kutibu ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.

Lakini jaribio la dawa hiyo nchini Uchina limeonesha kuwa dawa hiyo haikufanikiwa, kwa mujibu wa waraka uliochapishwa kimakosa na Shirika la Afya Duniani (WHO).


Dawa hiyo haikuboresha hali za wagonjwa au kupunguza kiwango cha virusi katika damu, ulisema waraka huo.

Kampuni ya Marekani inayotengeneza dawa hiyo, Gilead Sciences, imesema kuwa waraka huo ulipotosha uchunguzi wake.

Kipi tunachokifahamu kuhusu utafiti huo?
Taarifa juu ya kushindwa kwa jaribio la dawa hiyo ilisambaa baada ya WHO kutuma maelezo katika kanzidata (hofadhi ya kumbukumbu za kimtandao) yake ya kitabibu , na baadae kuondosha data hizo.


WHO imethibitisha kuwa ripoti hiyo ya muswada iliwekwa mtandaoni kimakosa.

Taarifa hiyo inaonesha kuwa kuwa watafiti waliwafanyia uchunguzi wagonjwa 137, wakawapatia dawa 158 na kulinganisha mafanikio na waliosalia 79, ambao walipewa dawa isiyo na kemikali ya placebo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho