Posts

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Image
Nchi za Rwanda na Nigeria kuanzia leo Jumatatu zimeanza kulegeza masharti ya amri ya kusalia ndani kwa wananchi wake kama sehemu ya mapambano dhidi ya corona. Nchini Rwanda marufuku hiyo ilikuwa imewekwa nchi nzima, huku Nigeria marufuku hiyo ilihusisha ndani katika mji mkuu wa Abuja, na mji mkubwa kabisa wa Lagos, katika jaribio la kupunguza athari ya kiuchumi barani Afrika. Nchi hizo mbili, zinaungana na mataifa mengine ya Afrika kama Ghana, Afrika Kusini na Kenya ambayo pia yamelegeza baadhi ya masharti makali ya hatua hizo za watu kusalia ndani. Mataifa kadhaa ya Afrika yamechukua hatua ya kuweka marufuku hiyo toka mlipuko wa virusi hivyo kuingia barani na kuonesha hatari ya maambukizi ya ndani ya jamii. Uganda pia inatarajiwa kutangaza kulegeza masharti kesho. Raisi Museveni anatarajiwa kulihutubia taifa hilo jioni ya leo. Baadhi ya shughuli za kibiashara zinatarajiwa kufunguliwa japo shule zinatarajiwa kuendelea kufungwa mpaka hapo itakapotangazwa. Japo hatari ya virusi ingalipo,...

Marekani yaidhinisha dawa ya dharura kwa wagonjwa wa virusi vya Corona

Image
Marekani imeidhinisha majaribio ya dawa ya dharura kutumika kwa wagonjwa wenye virusi vya corona, wakati majimbo zaidi nchini humo yakilegeza masharti ya kutotoka nje licha ya vifo vitokanavyo na virusi hivyo kuzidi kuongezeka. Kuidhinishwa kwa dawa hiyo ni hatua ya hivi karibuni ya juhudi za dunia kupata tiba kamili na chanjo ya virusi vya corona vilivyowaacha nusu ya watu duniani wakibakia nyumbani, kuutikisa uchumi wa dunia na kuwaambukiza watu zaidi ya milioni 3.3 ulimwenguni. Dawa hiyo inayojulikana kama Remdesivir, iliyotengenezwa kupambana na ugonjwa wa ebola iliidhinishwa baada ya majaribio kadhaa kuonesha imewasaidia wagonjwa mahututi wa COVID 19 kupata nafuu. Marekani ina wagonjwa milioni 1.1 wa virusi vya corona na kurekodi vifo 65,000 hali inayomfanya rais Donald Trump kuwa mbioni kubadili hali wakati taifa hilo lilio na uchumi mkubwa duniani likirekodi idadi kubwa ya watu waliokosa ajira kutokana na janga la virusi hivyo.

Sierra Leone: Waziri aendesha kikao akiwa na mtoto mgongoni

Image
Mara ya kwanza ilionekana kama picha nzuri iliyotumwa kwenye ukurasa wa Twitter kuwachangamsha watu katika nyakati hizi za corona. Lakini wakati ilipogundulika kuwa mwanamume huyo aliyeshirikisha umma picha ya binti yake mwenye umri wa miezi 10 akiwa amefungwa mgogoni mwake wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao alikuwa ni waziri wa elimu wa Sierra Leone, gumzo liligeuka kuwa la majukumu ya kijinsia. David Moinina Sengeh alisema kuwa alitaka kutoa mfano kwa wanaume wengine. Ameiambia BBC kuwa ni nadra sana kumuona mtoto kwenye mgongo wa baba katika nchi yake. Bila shaka, picha ya mwanamke mwenye mtoto mgongoni haijawahi kuwa kitu cha kushangaza jambo ambalo waziri huyo mwenye umri wa miaka 33 anaafiki.

Rais Magufuli salamu za Mei Mosi ” Tuchape kazi Ugonjwa usiturudishe nyuma”Rais Magufuli salamu za Mei Mosi ” Tuchape kazi Ugonjwa usiturudishe nyuma”

Image
Rais Dkt John Magufuli ametoa wito kwa waajiri kutotumia ugonjwa wa Corona kama kigezo cha kuwanyanyasa wafanyakazi. Katika salamu zake kwa Wafanyakazi katika siku hii ya Mei Mosi amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wafanyakazi katika ujenzi wa Taifa na itaendelea kusimamia maslahi yao na kuboresha mazingira yao ya kazi. Mwaka huu sherehe hazitafanyika ili kuepusha mikusanyiko ya watu ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Lukamba: “Diamond ni hatari kwa kujifukiza, Mama yake ndio fundi tunaenda mmoja mmoja tusiambukizane Corona”

Image
Mpiga picha wa msanii wa Bongo Fleva @diamondplatnumz @lukambaofficial ameeleza jinsi Boss wake @diamondplatnumz anavyojifukiza kwa lengo la kujikinga na Corona. Lukamba ameongeza kuwa @diamondplatnumz ni hatari sana kwa kujifukiza maana @mama_dangote ndio fundi wa mambo hayo “Tunajipiga nyungu mmoja mmoja kuhofia kuambukizana Corona.

RC Makonda atoa msaada wa mabati yenye gharama ya mil 476 kuhudumia nyumba 1000

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane, mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka. RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko. na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani* baada ya kukosa makazi ya kuishi* hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya *pole kwa adha waliyoipata.* Aidha *RC Makonda* amewapa *siku 10 Wakuu wa Wilaya* kuhakikisha *wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.* Aidha *RC Makonda* amesema *athari zinazoonekan...

Mfahamu Irrfan Khan, Mcheza filamu maarufu India aliyepoteza maisha

Image
Muigizaji huyo maarufu kutoka tasnia ya filamu za Kihindi (Bollywood) aliyetamba katika filamu za ‘Slumdog Millionaire’ na ‘Jurassic World’ amefariki leo asubuhi akiwa na miaka 53. Mwaka 2018, alitangaza kuwa na saratani katika mfumo wa tezi zinazotengeneza homoni (Endocrine Tumour). Tangu jana amekuwa kwenye Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) hospitali kutokana na bakteria kwenye utumbo ‘Colon Infection’. Mwaka 2013, alishinda tuzo ya Kitaifa ya Filamu za India kutokana na filamu ya Paan Singh Tomar. Filamu nyingine alizotamba nazo ni Lunchbox, The Namesake, New York, I Love You na Hindi Medium. Ya mwisho, Angrezi Medium imetoka mwezi uliopita. Khan amezikwa katika makaburi ya Versova Kabristan huko Mumbai muda mfupi baada ya taarifa zake za kifo kutolewa. Familia, ndugu na marafiki wa karibu ndio wamehudhuria.