Sierra Leone: Waziri aendesha kikao akiwa na mtoto mgongoni



Mara ya kwanza ilionekana kama picha nzuri iliyotumwa kwenye ukurasa wa Twitter kuwachangamsha watu katika nyakati hizi za corona.

Lakini wakati ilipogundulika kuwa mwanamume huyo aliyeshirikisha umma picha ya binti yake mwenye umri wa miezi 10 akiwa amefungwa mgogoni mwake wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao alikuwa ni waziri wa elimu wa Sierra Leone, gumzo liligeuka kuwa la majukumu ya kijinsia.

David Moinina Sengeh alisema kuwa alitaka kutoa mfano kwa wanaume wengine.

Ameiambia BBC kuwa ni nadra sana kumuona mtoto kwenye mgongo wa baba katika nchi yake.

Bila shaka, picha ya mwanamke mwenye mtoto mgongoni haijawahi kuwa kitu cha kushangaza jambo ambalo waziri huyo mwenye umri wa miaka 33 anaafiki.

Comments

Popular posts from this blog

MUONGOZO WA HATUA KWA HATUA :KUTENGENEZA SABUNI BORA ZA MAJI

HISTORIA YA OSAMA BIN LADEN KUZALIWA MPAKA KUFA

Yaelezwa huyu ndio mwanamke aliyepigwa busu mara nyingi zaidi duniani