Urithi utakaoishi alioacha Mkapa
WAKATI Afrika na dunia ikiendelea kumlilia Rais mstaafu Benjamin Mkapa (81) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Julai 24, viongozi mbalimbali wameelezea mchango wake kwa taifa wakisema ni urithi utakaoendelea kuishi baada ya yeye kumaliza safari yake duniani. Mkapa ambaye anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lupaso Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Juni 29, mbali na marais mbalimbali na viongozi wengine wa kimataifa ambao wameeleza kumkumbuka Mkapa kwa mchango wake wa kidiplomasia, viongozi wengine nchini pia wameeleza mambo ambayo yatazidi kukumbukwa daima. Mkapa aliyeshika nyadhifa mbalimbali kabla ya mwaka 1995 alipokuwa Rais, katika uongozi wake anatajwa kama mtu aliyejenga mifumo ya kitaasisi, kuinua sekta binafsi, kuanzisha taasisi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), kuanzisha uchimbaji mkubwa wa madini, kuinua diplomasia ya kiuchimi na kuboresha mfumo wa elimu uliosaidia watoto wengi kuanza kuandikishwa shuleni na elimu ya juu. Kwa mujibu wa viongozi m