Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, 81, afariki

Aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin Mkapa amefariki. Rais Mkapa aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa katika hospitali moja mjini Dar es Salaam.
Rais John Magufuli alitangaza kuhusu kifo cha Mkapa, ambaye alikuwa rais wa awamu ya tatu, kupitia taarifa fupi ya moja kwa moja kutoka Ikulu mwendo wa saa sita na dakika ishirini na tano saa za Afrika Mashariki.


"Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa. Mzee wetu, Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa amefariki akiwa hospitalini mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa," alisema Rais Magufuli.

"Tuendelee kumuombea Mzee Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," aliongeza.

.Kabla ya kuwa rais Mkapa alikuwa miongoni mwa wanadiplomasia waandamizi wa Tanzania akishika nafasi kama waziri wa mambo ya nje na balozi wa Tanzania katika utawala rais wa kwanza Jwa Mwalimu ulius Nyerere na rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.


Wakati wa uongozi wake Mkapa alisifiwa kwa kuweka taratibu na kanuni nyingi za shughuli za kiserikali kufanya idara za serikali zifanye kazi kwa ufasaha zaidi.

Kimataifa Mkapa alikuwa miongoni mwa viongozi waliohusika sana kwenye juhudi za kiuchumi na kutatua migogoro barani Afrika na katika ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za kusini-kusini.

Mara ya mwisho Mkapa alionekana hadharani wiki mbili zilizopita mjini Ddodoma katika mkutano wa taifa wa chama tawala cha mapinduzi CCM kilichomteua Rais Magufuli kugombania awamu ya pili ya uongozi nchini katika uchaguzi wa Oktoba 28

"Mzee Mkapa daima atakumbukwa kwa juhudi zake za upatanishi katika eneo la Afrika Mashaiki na Kati," alisema Profesa Patrick Nighula, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha South Carolina na mchambuzi wa masuala ya siasa, katika mahojiano na Sauri ya Amerika siku ya Alhamisi.

Mkapa, ambaye alikuwa rais wa Tanzania kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2005, alizaliwa Novemba 12, 1938. Amemuacha mjane, Anna Mkapa, na watoto.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho