TAFAKARI
Siku moja kundi la watu 50 walikuwa wakihudhuria semina moja.
Ghafla mwezeshaji akaacha kufundisha na kutoa zoezi ambalo walitakiwa kulifanya kwenye makundi aliyoyagawa.
Baada ya hapo akampa kila mtu puto na kumwambia alipulize lijae hewa na kuliandika jina lake kisha wakayakusanya na kuyaweka kwenye chumba kimoja.
Walipoyaweka kwenye kile chumba akawapa zoezi la pili kuwa kwa pamoja watumie dakika tano ambapo kila mtu awe amefanikiwa kulitafuta puto lenye jina lake.
Waliingia mle ndani kila mtu akawa busy akijaribu kulitafuta puto lake lakini hakuna aliyefanikiwa na dakika tano zaikaisha huku kila mtu akiwa hana puto mkononi.
Mwezeshaji akasema tena haya sasa kila mtu aingie na alichukue puto lolote na kumpa mwenye jina lake.
Wakaingia na haikufika hata dakika ya nne kila mtu akawa ameshapata puto lake na kakaa kwenye kiti chake.
Mwenzeshaji akawaambia hongereni sana, na huu mfano unaendana sana na maisha yetu ya kila siku, ambapo watu wako busy kuitafuta furaha katika maisha yao bila kujua furaha hiyo ipo wapi au wataipata wapi.
Furaha zetu zipo katika furaha za watu wenigne, wape furaha yao nawe utapata furaha yako.
Na hili ndilo kusudio na hitaji kuu la kila binadamu
Wewe unatafuta nini katika maisha?
Comment FURAHA na kisha share kama nawe waamini bila ya furaha hakuna mafanikio na ubunifu kwani mwili unakuwa katika hali ya unyonge na kusababisha kutokuwa na ujasiri wa kujituma.
Furaha inatakiwa sehemu zote: Nyumbani, kazini, mtaani, shuleni na kila sehemu katika maisha yetu
Comments
Post a Comment