Diamond, Zuchu na Nandy watikisa tuzo za Afrimma
Usiku wa kuamkia leo kulifanyika tuzo kubwa zinazofanyika kila mwaka barani Afrika ambazo ni tuzo za Afrimma.
Tuzo hizi hutafuta wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka kupitia kazi zao kama zilivyo tuzo zingine na baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutajwa/kuwania tuzo mwaka huu wengine kutoka Tanzania na mataifa mengine barani Afrika.
Kwa bahati nzuri tuzo hizo zilitolewa usiku wa kuamkia leo na baadhi ya wasanii kufanikiwa kushinda pia kwa upande wa Tanzania wakipata nafasi wasanii watatu tu. @diamondplatnumz aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki ‘Best male East Africa’ kwenye tuzo hizo za Afrimma.
Msanii mwingine kutoka Tanzania akiwa ni @officialzuchu ameshinda tuzo ya Msanii bora chipukizi ( Best Newcomer) lakini pia Nandy akishinda tuzo ya Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki ‘Best Female East Africa’
Mbali na hao wasanii wengine walioshinda nje ya Tanzania ni @masterkgsa amabye wimbo wake aliomshirikisha @nomcebo_zikode ‘Jerusalema’ umechaguliwa kuwa wimbo Bora wa Mwaka (Song of the Year) huku Rema akishinda tuzo ya ‘Best Male West Africa’
Mbali na hao wengine ni Staa kutoka chini Nigeria @symplysimi ameshinda tuzo ya ‘Best Female West Africa’ lakini pia Msanii wa muziki kutoka Nchini congo @fallyipupa01 ameshinda tuzo ya ‘Best male Central Africa’ na kwa mara nyingine Msanii wa muziki kutoka Nchini Afrika Kusini @masterkgsa Ameshinda tuzo ya Msanii bora wa mwaka (Artist of the Year)
Kutoka Afrika kusini Nasty C akishinda tuzo ya Rapper bora wa mwaka, hao ni baadhi ya wasanii walioshinda tuzo ya AFRIMMA kwa mwaka 2020.
Comments
Post a Comment