Balozi wa Uingereza avua barakoa akimpongeza Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho, Ikulu jijini Dar es Salaam ni David William Cancar (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza hapa nchini), Muhammad Saleem (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Pakistan hapa nchini) na Didier Chassot (aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uswisi hapa nchini).

Balozi wa Uingereza hapa nchini, David William Cancar amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri ambapo Tanzania kwa kufanikiwa kuingia katika uchumi wa nchi za kipato cha kati, kusambaza umeme kwa kasi kubwa, kutoa elimu bure, kujenga miundombinu hasa barabara.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na Rais Magufuli, tunatazamia kukuza zaidi uhusiano wa Uingereza na Tanzania hasa katika biashara, kwa sasa biashara yetu ni takribani Bilioni 390 kwa mwaka na pia tunachangia takribani Bilioni 800 kwa mwaka katika miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Tanzania. Matarajio yangu ni kuwa tutaongeza Zaidi,” 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho