UINGEREZA: Hii ndio dawa ya Corona iliyobainika kutibu baada ya majaribio
Shirika la Afya Duniani (WHO) limefurahishwa na matokeo ya awali ya majaribio ya dawa ya kutibu corona Uingereza yanayoonesha kwamba dawa ya dexamethasone, inaweza kuokoa maisha ya watu walio mahututi wanaougua ugonjwa wa Covid-19. Kwa wagonjwa wanaotumia mashine za kupumua, dawa hiyo ilionesha kwamba imepunguza idadi ya vifo kwa theluthi moja, na kwa wagonjwa wanaohitaji hewa ya oksijeni, idadi ya vifo ilipungua kwa humusi au moja ya tano kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa na WHO. Hata hivyo, faida ama uzuri wa dawa hiyo kulijitokeza kwa wagonjwa wanaoumwa sana kwasababu ya virusi vya corona wala sio kwa wenye athari za wastani za ugonjwa huo. Shirika la Afya Duniani (WHO) limefurahishwa na matokeo ya awali ya majaribio ya dawa ya kutibu corona Uingereza yanayoonesha kwamba dawa ya dexamethasone, inaweza kuokoa maisha ya watu walio mahututi wanaougua ugonjwa wa Covid-19. Kwa wagonjwa wanaotumia mashine za kupumua, dawa hiyo ilionesha kwamba imepunguza idadi ya vifo kwa theluth