Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho
George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46 ambaye mauaji yake na polisi mweupe yamembadilisha kuwa picha ya ulimwengu ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi, atazikwa leo mjini Houston, ambako alikulia.
Waombolezaji wengi walitengeneza ishara ya msalaba wakati wakikaribia jeneza la Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho wakati wengine wakipiga magoti au kuinamisha vichwa na kumuombea kimyakimya mtu ambaye amekuwa ishara ya karibuni ya vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Marekani.
Mwili wa George Floyd kuzikwa leo, maelfu wafurika kanisa la ‘The Fountain of Praise’ kutoa heshima za mwisho (+Picha)
Hamza Fumo6 hours ago 343
George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46 ambaye mauaji yake na polisi mweupe yamembadilisha kuwa picha ya ulimwengu ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi, atazikwa leo mjini Houston, ambako alikulia.
Public viewing for George Floyd underway in Houston - Houston ...
Waombolezaji wengi walitengeneza ishara ya msalaba wakati wakikaribia jeneza la Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho wakati wengine wakipiga magoti au kuinamisha vichwa na kumuombea kimyakimya mtu ambaye amekuwa ishara ya karibuni ya vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Marekani.
Staff slideshow: George Floyd public viewing on Monday, June 8 ...
Hafla hiyo ilikuwa ya mwisho katika msururu wa hafla zilizoandaliwa za kumuaga Floyd. Atazikwa leo katika mazishi ya faragha kando ya kaburi la mamake mjini Houston, ambako ndiko alikokulia.
Mjini Washington, wajumbe wa Democratic walipiga magoti na kusalia kimya kwa dakika nane na sekunde 46, muda alioutumia polisi mweupe kugandamiza shingo ya Floyd akitumia goti.
Wademocrat wamewasilisha mswada wa sheria za kuimarisha udhibiti wa polisi, ikiwa ni mojawapo ya masharti muhimu ambayo waandamanaji wanadai. Marekani imeshuhudia maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa ya kudai haki tangu mauaji ya Maetin Luther King Jr.
Polisi wengine watatu wa Minneapolis walifikishwa mahakamani wiki iliyopita wakikabiliwa na mashitaka ya kusaidia katika mauaji ya Floyd. Wote wanne wamefutwa kazi.
Comments
Post a Comment