Rais Magufuli: Ugonjwa wa Corona nchini umeondolewa kwa nguvu za Mungu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi wa dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu aepushe janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).
Rais Magufuli amesema Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake ni kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yamepungua, na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi za uzalishaji mali, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ugonjwa huo ungesababisha madhara makubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati alipokuwa akiendesha Harambee ya Papo kwa papo kwa ajili ya upanuzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 7 Juni 2020.

Katika Harambee hiyo jumla ya Shilingi Milioni 17 zilipatikana pamoja na mifuko 76 ya Saruji na Mhe. Rais Magufuli alichanga peke yake kiasi cha Shilingi Milioni 10.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MKWAWA AMBAYE ALIWAHI KUWA CHIFU WA UHEHE HISTORIA YA MKWAWA Mkwawa alikuwa kiomgozi wa jadi wa kabila la wahehe nchini Tanzania, ni moja kati ya viongozi shupavu wa jadi waliowahi kuishi duniani japo mapokeo yao yanaharibiwa taratibu na mabadiliko ya sayansi na technolojia lakini kumbukumbu zao hazitasahauliki hata vizazi vingi vijavyo. miongoni mwa machifu wanaotajwa kuwa na nguvu za kiutawala kwa kipindi hicho ni pamoja na kinjekitile ngwale wa songea aliyeongoza vita za majimaji, Mirambo wa Tabora nk PICHA YA MKWAWA

Nigeria, Rwanda ruksa kutoka nje, ni baada ya Lockdown

Mchungaji Kyashama “Upinzani kazi yao kuiongelea vibaya Serikali wanatia aibu, Rais Magufuli anapewa maono na Mungu”