Maandamano yazuka upya baada ya polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi
Kisa kingine cha polisi nchini Marekani kumpiga risasi na kumuua Mmarekani mwengine mweusi katika mji wa Atlanta Georgia wikendi hii, kimezusha ghadhabu na maandamano tena, pamoja na mjadala unaoendelea ulimwenguni kote wa kupinga ubaguzi wa rangi.
Maandamano yazuka upya baada ya polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi
Hamza Fumo5 hours ago 259
Kisa kingine cha polisi nchini Marekani kumpiga risasi na kumuua Mmarekani mwengine mweusi katika mji wa Atlanta Georgia wikendi hii, kimezusha ghadhabu na maandamano tena, pamoja na mjadala unaoendelea ulimwenguni kote wa kupinga ubaguzi wa rangi.
Man's death after police shooting outside Wendy's in Atlanta ...
Mkuu wa polisi wa Atlanta tayari amejiuzulu wadhifa wake kutokana na kisa hicho.
Kadhalika idara ya polisi ya Atlanta imesema, imemfuta kazi polisi mmoja kutokana na kifo hicho.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyetambuliwa kwa jina Rayshard Brooks alipigwa risasi siku ya Jumamosi, alipokataa kukamatwa baada ya kufeli katika vipimo vya kubaini hali yake au ikiwa ametumia mihadarati.
Kufuatia kifo chake maandamano yamezuka Atlanta na kwingineko nchini Marekani huku waandamanaji wakichoma moto mkahawa wa Wendy karibu na eneo alikouawa.
Kisa hicho kimejiri wiki chache baada ya mauaji ya George Flody ambayo yalichochea maandamano makubwa ulimwenguni kote.
Comments
Post a Comment