Posts

Showing posts from November, 2020

Tanzania vs Tunisia, tuiombe Taifa Stars – Rais TFF Wallace Karia.

Image
Rais wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati Cecafa na ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amewaomba Watanzania kuiombea timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars kuhakikisha hii leo usiku inachomoza na ushindi dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa ‘Group J’ mchezo wa kufuzu AFCON 2021 utakaopigwa uwanja wa Mkapa saa 4:00 usiku. Karia ambaye pia ni Rais wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati Cecafa amezungumzia mashindano ya Cecafa ya U20 yatakayoanza kutimua vumbi tarehe 22 katika Mkoa wa Arusha na Karatu nchini Tanzania. Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 2 Disemba na kushirikisha jumla ya timu tisa (9). Wallace Karia amesema dhana yake ni kuhakikisha ausambaza mchezo wa mpira wa miguu katika sehemu mbalimbali. ”Matarajio yangu katika kipindi changu tutaziacha timu zikiwa juu katika Rank ya FIFA tofauti tunavyotazamwa sasa hivi ziko chini. Tulichukua U17 Boys, mwaka jana tukachukua U20 Girls na mwaka huu tumekwenda k

Diamond, Zuchu na Nandy watikisa tuzo za Afrimma

Image
Usiku wa kuamkia leo kulifanyika tuzo kubwa zinazofanyika kila mwaka barani Afrika ambazo ni tuzo za Afrimma. Tuzo hizi hutafuta wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka kupitia kazi zao kama zilivyo tuzo zingine na baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutajwa/kuwania tuzo mwaka huu wengine kutoka Tanzania na mataifa mengine barani Afrika. Kwa bahati nzuri tuzo hizo zilitolewa usiku wa kuamkia leo na baadhi ya wasanii kufanikiwa kushinda pia kwa upande wa Tanzania wakipata nafasi wasanii watatu tu. @diamondplatnumz aliyeshinda tuzo ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki ‘Best male East Africa’ kwenye tuzo hizo za Afrimma. Msanii mwingine kutoka Tanzania akiwa ni @officialzuchu ameshinda tuzo ya Msanii bora chipukizi ( Best Newcomer) lakini pia Nandy akishinda tuzo ya Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki ‘Best Female East Africa’ Mbali na hao wasanii wengine walioshinda nje ya Tanzania ni @masterkgsa amabye wimbo wake aliomshirikisha @nomcebo_zikode ‘Jerusalema’ umechaguliwa kuwa wimbo B

HII NI KWA WANAOGOPA KUUMIZWA KATIKA MAPENZI

Image
Ni jambo lisilofichika kuwa wapo watu wengi wanaogopa kuumizwa katika mapenzi. Kuumizwa huku kunaweza kuwa kwa namna kadhaa kama vile kumpenda mtu halafu mtu husika asionyeshe kukujali, au kuwa katika mahusiano na mtu halafu mtu huyo baada ya muda fulani akakuacha na kuenda zake na mpenzi mwingine. Kwa mtazamo huu watu wanaogopa kuumizwa katika mapenzi wapo wa aina mbili; wale ambao wanaogopa hata kuwa na mpenzi kwa sababu ya kuogopa kuumizwa, na wale ambao wapo katika mapenzi lakini hawaamini kama wapo salama, maisha yao ni ya wasiwasi kuwa muda wowote mpenzi anaweza kumuacha ‘solemba’. Makala hii inachambua namna ya ‘kudeal’ na hofu ya kuumizwa katika mapenzi. Sababu za kuogopa: Mambo kadhaa yanaweza changia mtu kuogopa kuumizwa katika mapenzi. Zifuatazo ni baadhi: Mtu alishawahi kuachwa ‘solemba’ na mpenzi hapo kabla Mtu ameshuhudia rafiki, ndugu au jirani akiachwa ‘solemba’ Wivu uliopitiliza kwa mpenzi husika bila kuwa na sababu za msingi za wivu. Kuishi kwa kufuata matarajio ya wa